Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:47

Uamuzi mpya watolewa katika kesi ya Freddie Gray


Waandamanaji nje ya mahakama
Waandamanaji nje ya mahakama

Mahakama kuu iliamua kwamba ni lazima William Porter atoe ushahidi dhidi ya wenzake wakati akingoja kusikilizwa kesi ya Freddie Gray.

Mahakama kuu ya jimbo la Maryland nchini Marekani imetoa uamuzi kuwa afisa wa polisi, William Porter, kutoka jiji la Baltimore anaekabiliwa na shitaka la kumuua Freddie Gray wakati akiwa chini ya ulinzi wa polisi ni lazima atoe ushahidi dhidi ya wenzake wakati akingoja kusikilizwa kesi yake tena.

Afisa William Porter
Afisa William Porter

Gray aliekuwa na umri wa miaka 25 alipata majeraha ya uti wa mgongo akiwa amefungwa pingu ndani ya gari la polisi bila kuwa amevaa mkanda wa kiti cha gari mwezi Aprili mwaka jana ambapo alikufa wiki moja baadae.​

Mahakama hiyo ya rufaa haikutoa sababu za uamuzi huo lakini imesema kuwa itatoa taarifa baadaye. Mwakilishi mmoja wa mahakama hiyo amesema Potter atahitajika kutoa ushahidi dhidi ya baadhi ya maafisa wenzake waliohusishwa na kesi ya Freddie Gray.

XS
SM
MD
LG