Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:14

Republican na Democrat wapinga kauli ya Trump


Katika hali ya nadra ya umoja katika kipindi cha uchaguzi imejitokea baada ya Warepublikan na Wademokrat kumshutumu anayetazamiwa kuwa mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump kwa matamshi yake kuhusu asili ya jaji anayesimamia kesi ya chuo kikuu inayomkabili Bwana Trump.

Wanachama wa vyama vyote walipinga kauli ya bilionea huyo na kuiona kuwa ni ya ubaguzi wa rangi.

Bwana Trump alisema kwamba jaji wa mahakama ya mwanzo ya Marekani, Gonzalo Curiel, hatoweza kusimamia kesi yake kwa haki kwa sababu ya asili yake ya Mexico. Jaji huyo ni Mmarekani aliyezaliwa na kukulia katika jimbo la Indiana, hapa Marekani.

XS
SM
MD
LG