Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:10

Ushahidi watolewa katika hukumu ya Pistorius


Barry Steenkamp, father of Reeva Steenkamp, reacts as he hears the verdict at the North Gauteng High Court in Pretoria, Sept. 12, 2014.
Barry Steenkamp, father of Reeva Steenkamp, reacts as he hears the verdict at the North Gauteng High Court in Pretoria, Sept. 12, 2014.

Baba wa Reeva Steenkamp, mwanamke aliyeuliwa na mwanariadha mashuhuri wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, ametoa ushahidi wa kuhuzunisha mapema leo Jumanne wakati wa kikao cha kutoa hukumu ya mwanariadha huyo.

Barry Steenkamp amesema kuwa kifo cha bintie kilivuruga maisha yake pamoja na familia yake na kwamba Pistorius anafaa kulipia kosa lake.

Reeva Steenkamp alikuwa mwanfunzi wa sheria mwenye miaka 29 wakati alipouwawa na mpenzi wake mwanariadha mashuhuri.

Reeva Steenkamp
Reeva Steenkamp

Oscar Pistorius anaekabiliwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia kwa mauwaji hayo.

Pistorius aliketi akiwa ameinamisha kichwa chake wakati Bw Steenkamp alipokuwa akitoa ushahidi kwa mara ya kwanza tangu kesi hiyo ilipoanza 2014.

XS
SM
MD
LG