Keshi dhidi ya tajiri mkubwa wa ujenzi wa Vietnam Truong My Lan, imeanza kusikilizwa Jumanne katika mji wa Chi Minh City. Waendesha mashitaka wamesema kwamba Truong My Lan aliyekuwa mwenye kiti wa kampuni ya ujenzi ya Van Thinh Phat alitoa dola bilioni 12.5 za kimarekani kutoka kwenye benki ya Saigon Joint Commercial kati ya 2012 na 2022. Lan ambaye alikuwa mwenye hisani mkuu kwenye benki hiyo anasemekana kuchua fedha kwa kutumia mikopo bandia kupitia makampuni kadhaa yenye mashaka. Watu wengine 85 wameshitakiwa pamoja na yeye kuhusiana na kesi hiyo, akiwemo mume wake, ambaye ni mfanyabiashara tajiri wa Hong Kong wakiwemo waliokuwa wafanyakazi wa benki na maafisa wa serikali. Miongoni mwa maafisa wa serikali kuna mmoja anayedaiwa kupokea dola bilioni 5.2 kwa njia ya hongo. Karibu mawakili 200 wanahusika kwenye kesi hiyo. Ukubwa wa wizi unaodaiwa kufanyika kwenye kesi hiyo ni karibu asilimia 3 ya mapato ya ndani ya Vietnam mwaka 2022. Iwapo Lan atapatikana na hatia, basi hukumu yaka itakuwa ni kifo.
Forum