Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:45

Kerry hajakata tamaa na suluhisho la amani mashariki ya kati


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (L) akisalimiana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (L) akisalimiana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry.

Licha ya kuongezeka karibuni kwa ghasia kati ya waisrael na wapalestina na ukweli kwamba wawakilishi wa pande hizi mbili hawajapangiwa kuhudhuria kuanza tena kwa mazungumzo yanayosimamiwa na Ufaransa yenye lengo la kumaliza mgogoro kuna ishara za matumaini kwa upande ulioapishwa Jumatatu wa waziri wa ulinzi wa Israel, Avigdor Lieberman, ambaye alisema anaunga mkono suluhisho la mataifa mawili.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry hajakata tamaa ya kupatikana kwa mkataba wa kudumu wa kumaliza mgogoro wa waisrael na wapalestina baada ya utaratibu wa mazungumzo ya amani aliyoyaongoza kuvunjika mwezi April mwaka 2014.

Alikuwa makini na mtazamo wake wa mataifa mawili kwa watu kuishi pamoja kwa amani na usalama hata baadhi wakiita mpango usiozaa matunda na pande mbili kuu zilizohusika kila mmoja alikataa kuzungumza na mwenzie.

XS
SM
MD
LG