Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 19:51

Kerry atetea shambulizi la Navy SEAL, Llibya


Kikosi maalumu cha jeshi la Marekani, Navy SEAL
Kikosi maalumu cha jeshi la Marekani, Navy SEAL
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry anatetea shambulizi lililofanywa na kikosi maalumu cha Marekani kumkamata kiongozi mwandamizi wa al-Qaida nchini Libya akisema operesheni hiyo ilikuwa “halali na muafaka”.

Serikali ya Libya inaitaka Marekani kuelezea kuhusu kile inachokiita “utekaji nyara” wa Abu Anas al-Libi ndani ya ardhi ya Libya tukio lililofanyika siku ya Jumamosi.

Kerry alisema Jumatatu pembeni ya mkutano wa kieneo huko Indonesia kwamba madai ya Libya hayana msingi na kwamba Libi atafikishwa kwenye mahakama ya sheria.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani inasema Libi amehamishwa kwenda “eneo salama” nje ya Libya.

Mahakama moja ya Marekani inamfungulia mashtaka Libi kwa kuhusika kwake katika ulipuaji mabomu uliofanyika mwaka 1998 katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania. Mashambulizi hayo yaliuwa zaidi ya watu 200 na kuwajeruhi 5,000 wengine.

Saa kadhaa kabla ya kukamatwa Libi siku ya Jumamosi majeshi maalumu ya Marekani pia yalishambulia kituo cha majini cha al-Shabab chenye uhusiano na al-Qaida nchini Somalia.

Maafisa wa Marekani walisema kikosi maalumu cha jeshi la Marekani, Navy SEAL, kiliuwa wanamgambo kadhaa wa al-Shabab katika mapigano ya risasi baada ya kuja kwenye mwambao katika mji wa Barawe.
XS
SM
MD
LG