Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 09:06

Kerry ashindwa kuleta mpango wa kusimamisha mapigano Syria


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amerejea nyumbani mikono mitupu akishindwa kufikia mkataba wa makubaliano na wenzake wa Russia wa kusimamisha mapigano nchini Syria.

Shauri hilo halikufanikiwa licha ya baada ya kupindi kirefu cha majadiliano ya masuala ya kideplomasia.

Nchi hizo mbili bado zinahitaji kutatua kile kinachoitwa masuala ya kiufundi na majadiliano baina ya Marekani na wapatanishi wa Russia yanatarajiwa kuendelea wiki hii kwa mujibu wa maafisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Nje ya mkutano wa G-20 mjini Hangzhou, China, marais wa Russia na Marekani walifanya mazungumzo kuhusu Syria.

Rais Barack Obama wa Marekani ameyaelezea mazungumzo hayo kama ya kibiashara na kusema yalikuwa ya kujenga licha ya kutofikia muafaka.

XS
SM
MD
LG