Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 21:12

Kenya:Watu 28 wajeruhiwa na mlipuko Nairobi


Rais wa Kenya Mwai Kibaki

Taarifa zinasema bado haijagundulika chanzo cha mlipuko huo uliosababisha kituo cha mafuta kuungua moto.

Maafisa wa usalama nchini Kenya wanasema takriban watu 28 wamejeruhiwa jumapili na mlipuko mjini Nairobi na kusababisha kituo cha mafuta kuungua moto.

Mashahidi wanasema mlipuko ulizuka mida ya saa tano asubuhi saa za Nairobi karibu na barabara ya kirinyaga mjini humo.

Majeruhi walikimbizwa katika hospitali jirani ambako wengi walitibiwa kutokana na majeraha ya kuungua moto vibaya.

Maafisa wa usalama bado hawajaamua kama mlipuko huo ulikusudiwa au ilikuwa bahati mbaya.

Kenya imekumbwa na milipuko ziku za nyuma hasa mwezi desemba katika basi ambalo lilikuwa linatarajia kusafiri kwenda mji mkuu wa Uganda , Kampala Takriban watu wawili walikufa katika mlipuko huo.

Kundi la wapigani la somalia al- shabab limerudia kutishia kushambulia Kenya kutokana na uungaji mkono wake katika serikali ya Somalia inayoungwa mkono pia na umoja wa mataifa.


XS
SM
MD
LG