Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 16:07

Kenyatta, Xi wafanya mazungumzo


Rais Uhuru Kenyatta

Rais wa China Xi Jinping, amekutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, ambaye yuko China akihudhuria mkutano wa ushirikiano wa kimataifa kuhusu ujenzi wa reli na barabara.

Hii ni mara ya tatu Kenyatta kukutana na Xi Jinping katika kipindi cha mwaka mmoja, ambapo Xi Jinping amesema mkutano huo ni muhimu kwa ajili ya kuboresha uhusiano mwema kati ya Kenya na China.

Xi Jinping, amesema anafurahishwa na jinsi Kenyatta alivyo na msimamo thabithi dhidi ya shutuma zinazotolewa kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na ushirikiano wa China na Afrika.

Viongozi hao wamekubaliana kuimarisha uhusiano wao katika kufanikisha miradi mbalimbali.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG