Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Jumatatu amewafutia adhabu ya kifo takriban wafungwa 2,747 ambao walikuwa wanasubiri kunyongwa na hivyo hivi sasa watatumikia kifungo cha maisha jela.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa, Kenyatta alitia saini waraka wa kuwafutia adhabu hiyo wakati wa sherehe ambazo zilifanyika kwenye makazi yake rasmi na pia kuwasamehe wafungwa 102 ambao wamekuwa wakitumikia vifungo kwa muda mrefu.
Amnesty International imefurahishwa na hatua hiyo na kuisihi kenya kufuta rasmi adhabu ya kifo. Kenya haijawahi kunyonga mtu yoyote tangu mwaka 1987. Uamuzi wa kuwafutia adhabu ya kifo unaifanya kenya ikaribie kuifikia jumuiya ya mataifa ambayo imefuta adhabu ya kifo kwa vile ni ya kinyama na si kitendo cha kibinadamu, alisea Muthoni Wanyeki mkurugenzi wa haki za binadamu katika taasisi hiyo.