Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:08

Kenyatta atangaza majina zaidi ya mawaziri-wateule


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza majina 12 zaidi ya wajumbe wa baraza lake la mawaziri ambalo linajumuisha wanawake sita katika nyadhifa muhimu kama vile wizara ya ulinzi na mambo ya nje.

Akizungumza nje ya Ikulu Alhamis wakati alipowatambulisha wateuliwa hao Rais Kenyatta alisema pendekezo lake la majina kwenye baraza la mawaziri linaelezea nia ya dhati ya utawala wake katika kufanya kazi na makundi mchanganyiko.

“Kama ninavyofahamu, hakuna wizara ya vijana, hakuna wizara ya wanawake, lakini kutakuwa na vijana na wanawake waliohusishwa katika kila kiwango cha ufanyaji maamuzi kwenye kila uwakilishi katika kuendeleza nchi yetu.”
Mahojiano na M Ole Tiampati - 3:07
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:07 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bwana Kenyatta ambaye alichukua madaraka wiki mbili zilizopita amekuwa akitangaza uteuzi wake kwa awamu watu ambao wanaweza kuingia kwenye baraza la mawaziri, huku nchi ikiwa na shauku ya kuona sura mpya katika utawala wake. Miongoni mwa majina yaliyotangazwa Alhamis alikuwepo Raychelle Omamo, ambaye kama uteuzi wake ukipita atakuwa waziri wa ulinzi.

Omamo ana uzoefu wa kidiplomasia kama balozi wa zamani wa Kenya nchini Ufaransa, Ureno na Holy See. Pia alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Kenya Law Society.

Kama uteuzi wake ukipitishwa na bunge, Omamo ataongoza jeshi la Kenya ambalo lina wanajeshi wake nchini Somalia. Jumatatu Kenyatta alimteuwa Amina Mohammed kuongoza wizara ya mambo ya nje. Atakuwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafasi hiyo katika historia ya Kenya.
XS
SM
MD
LG