Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 01:44

Kenyatta atangaza baadhi ya mawaziri


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza baraza lake jipya la mawaziri na kuwarudisha mawaziri sita wa zamani katika baraza hilo.

Kati ya wale waliorudishwa ni pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Joe Machiru, Waziri wa Elimu, Fredd Matiang’i ambaye pia anakaimu nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani. Wengine ni Waziri wa Fedha Henry Rotich, Waziri wa Utalii Najib Balala, Waziri wa Usafirishaji na Miundo Mbinu, James Wainaina Macharia na Waziri wa Nishati, Charles Keter.

Pia mawaziri watatu wapya katika baraza hilo ambao bado wizara zao hazijatajwa ni aliyekuwa mkurugenzi wa makossa ya jinai Keriako Tobiko, Gavana wa zamani wa Marsabit governor Ukur Yatani na seneta wa zamani wa TurkanaJohn Munyes.

Aliyekuwa Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua amechaguliwa kuwa msimamizi wa fedha Ikulu.

Katika mabadiliko yaliofanywa na Rais Kenyatta amemuondoa Ndegwa Muhoro katika nafasi ya Mkuu wa Upelelezi na kumchagua George Kinoti kukaimu nafasi hiyo.

XS
SM
MD
LG