Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:04

IEBC yachelewesha kutangaza mshindi wa uchaguzi mkuu Kenya


Rais mteule wa Kenya Uhuru Kernyatta akifuatana na mkewe Margaret Wanjiru Gakuo, (kulia) ,akipiga kura kaika kituo cha shuke ya msingi Mutomo Gatundu, kaskazini mwa Nairobi, Kenya, March 4, 2013.
Rais mteule wa Kenya Uhuru Kernyatta akifuatana na mkewe Margaret Wanjiru Gakuo, (kulia) ,akipiga kura kaika kituo cha shuke ya msingi Mutomo Gatundu, kaskazini mwa Nairobi, Kenya, March 4, 2013.
Tume huru ya uchaguzi ya Kenya IEBC inachelewesha kutangaza mshindi wa uchaguzi wa rais baada ya muungano wa CORD kuewasilisha malalamiko ya kasoro katika utaratibu wa kuhesabu kura.

Awali tume ilipanga kumtaja mshindi wa uchaguzi wa kihistoria saa 5 mchana saa za Kenya siku ya Jumamosi lakini CORD inadai kuna kura 170 elfu ambazo hazijahesabiwa na kuna kasoro kadhaa katika utaratibu wa kuhesabu.

Jana usiku IEBC ilitangaza matokeo rasmi ya awali ambapo Uhuru Kenyatta wa muungano wa Jubilee amepata ushindi akiwa na asili mia 50.03 za kura na kumwezesha kutajwa msindi bila ya kwenda kwa duru ya pili.

CORD inadai kasoro zilizopo zinaweza kusababisha kuwepo na duru ya pili na ikiwa hawatapata jibu la kuridhisha watakwenda mahakama kuu.

Jana usiku mara baada ya matokeo kutangazwa watu walishuka katika njia za miji mikuu ya ngome za muungano wa Jubilee. Wakenya wote wanataka amani idumishwe. Huko magharibi ya Kenya ngome ya Raila Odinga inaripotiowa kuwa hali ya huzuni.
XS
SM
MD
LG