Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:38

Kenyatta azuru Cuba kuimarisha mahusiano


Rais Uhuru Kenyatta akikaribishwa na afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Cuba alipowasili mjini Havana, Cuba, kuanza ziara rasmi.
Rais Uhuru Kenyatta akikaribishwa na afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Cuba alipowasili mjini Havana, Cuba, kuanza ziara rasmi.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliwasili nchini Cuba Alhamisi kuanza ziara rasmi ya siku tatu. Kupitia taarifa, msemaji wa ikulu ya Kenya, Manoah Esipisu, alisema kuwa ziara hiyo itaangazia  masuala ya Afya, biashara na utamaduni.

Alisema kuwa Kenya inatathmini mfumo wa afya wa Cuba katika juhudi za kuimarisha sekta yake katika nyanja hiyo, ambayo ni moja ya nguzo nne muhimu zinazoangaziwa na utawala wa Kenyatta katika muhula wake wa pili madarakani.

Cuba ina mfumo wa afya unaosifika duniani kote.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani, kila daktari mmoja anahudumia watu 150 nchini Cuba, ikilinganishwa na Kenya, ambako kila watu 16,000 wanahudumiwa na daktari mmoja.

Kenyattta anatarajiwa kukutana na rais Raul Castrol na vile vile kufungua rasmi ubalozi wa Kenya nchini Cuba. Ubalozi wa Kenya nchini Cuba ulizinduliwa mnamo mwaka wa 2016.

XS
SM
MD
LG