Wakenya wengi wameendelea kuelezea wasiwasi wao kufuatia hatua ya serikali nchini humo kutotoa habari kamili kufuatia shambulizi lililowaua wanajeshi wa Kenya nchini Somalia. Sauti ya Amerika imezungumza na Steven Waweru, ambaye ni mchambuzi wa maswala ya Kisiasa nchini Kenya na kwanza kumuuliza hisia za baadhi ya watu nchini humo kuhusu hoja hiyo ni zipi.