Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 18:35

Jengo laanguka Nairobi, lauwa watu 2 wengi wakwama


Jengo laanguka Nairobi, lauwa watu 2 wengi wakwama

Maafisa wa usalama wanasema jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka jumanne lakini hawajasema chanzo chake.

Maafisa nchini Kenya wanasema jengo moja lililoporomoka katika mji mkuu wa Nairobi limesababisho vifo vya watu wawili na wengine kukwama ndani.

Maafisa wa usalama wanasema jengo hilo la ghorofa sita lilikuwa katika ujenzi limeporomoka leo.

Kundi la uokozi liko katika eneo la tukio kutafuta waliokwama ndani ya mabaki ya jengo hilo.

Shirika la msalaba mwekundu la Kenya limesema idadi kadhaa ya watu wamejeruhiwa baada ya jengo hilo kuporomoka ingawa halikusema ni watu wangapi.

Jengo hilo la ghorofa sita liko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mashariki mwa Nairobi . Chanzo cha ajali hiyo bado hakijaelezwa.

XS
SM
MD
LG