Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:33

Kenya yauwa wanamgambo Somalia


Majeshi ya Kenya katika bustani ya uhuru Park Nairobi Oktoba 20, 2011
Majeshi ya Kenya katika bustani ya uhuru Park Nairobi Oktoba 20, 2011

Kenya yafanya mashambulizi ya angani Somalia

Afisa wa Kenya anasema majeshi ya nchi hiyo yamefanya mashambulizi ya angani kusini mwa Somalia na kuuwa dazeni ya wanamgambo wenye ushirika na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida katika juhudi zinazoendelea kutokomeza wanamgambo nchini Somalia. Msemaji wa jeshi kanali Cyrus Oguna, aliwaambia waandishi habari Jumamosi kuwa wanamgambo wapatao 60 wa kundi la al-Shabab waliuawa Ijumaa katika mji wa Garbaharey katika eneo la Gedo huko Somalia. Alisema majeshi ya Kenya yalipashwa habari juu ya eneo walilokuwa wanamgambo hao na kisha kuwashambulia. Anasema idadi ya waliouawa inategemewa kuongezeka. Majeshi ya Kenya yaliingia Somalia mwezi Oktoba kupambana dhidi ya kundi la al –Shabab linalodhibiti eneo kubwa na kusini na katikati mwa Somalia na ambalo Kenya inalaumu kwa utekaji nyara ndani ya ardhi yake na kwenye mpaka baina ya nchi hizo mbili. Habari kutoka Uingereza zimesema leo Jumamosi kuwa London inaamini Kenya inakabiliwa na tishio la kushambuliwa na magaidi. Ofisi inayohusika na maswala ya nje huko London, inasema uingereza inaamini kuwa magaidi wamo katika hatua za mwisho mwisho za kupanga njama za kuishambulia Kenya.

XS
SM
MD
LG