Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:40

Kenya yaunga mkono uamuzi wa Uingereza kujitoa EU


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais Kenyatta amesema bila kujali matokeo ya wananchi wa Uingereza wameamua wametoa sauti yao imesikika.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema nchi hiyo itaunga mkono uamuzi wa Uingereza kuondoka kwenye umoja wa Ulaya

Rais Kenyatta amesema bila kujali matokeo ya wananchi wa Uingereza wameamua wametoa sauti yao imesikika.

Kenya kama kawaida itaendelea kudumisha uhusiano wake wa kihistoria na Uingereza huku ikeendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya ulio na uthabiti” . Hayo yaliandikwa katika taarifa ya Ikulu iliyosomwa na msemaji wa ikulu ya Kenya Manoa Esipisu.

Kwa mujibu wa jarida la The Star rais Kenyatta amewathibitishia wananchi kwamba hakutakuwa na athari za mara moja na kusema mazungumzo ya pande mbili kati ya nchi hizo mbili yataendelea bila kujali athari yoyote.

“Athari za mara moja kwa Kenya ni kidogo , lakini hata hivyo kutokana na kuondoka huko kutakuwa na haja kwa Kenya na jumuiya ya Afrika mashariki kufanya makubaliano tofauti ya kibiashara na Uingereza. Makubaliano yetu ya sasa yako ndani ya Umoja wa Ulaya.

XS
SM
MD
LG