Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 11:19

Kenya yasema inatarajia kupata mkopo kutoka China

Rais wa Kenya William Ruto akihutubia wakati wa kikao cha Ngazi ya juu kwa Wakuu wa Nchi na Serikali katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa mjini Dubai Desemba 1, 2023.AFP.
Rais wa Kenya William Ruto akihutubia wakati wa kikao cha Ngazi ya juu kwa Wakuu wa Nchi na Serikali katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa mjini Dubai Desemba 1, 2023.AFP.

Gavana wa benki kuu ya kenya Kamau Thugge   amesema leo jumatano kwamba nchi yake inatarajia kupata mkopo mpya wa karibu dola bilioni moja kutoka Uchina mnamo mwaka huu wa fedha na inaweza kutumia fedha hizo kulipa deni lake la Eurobond ambayo inatarajiwa kuanza kulipwa mwezi june mwakani.

Mkopo huo ulitangazwa kwa mara ya kwanza na maafisa wa kenya mwezi Oktoba ikionesha mabadiliko ya msimamo wa serikali ya Rais William Ruto kuhusiana na kukopa kutoka China baada ya kukosoa mikopo wakati wa kampeni zake wakati wa uchaguzi wa mwaka jana.

Thugge ameuwambia mkutano wa waandishi habari hii leo jumatano kwamba benki kuu iko kwenye majadiliano na serikali ya Chijna hivi sasa juu ya mkopo huo lakini muda wa kuupokea haujaamuliwa bado. Amesema wanatarajia kuupata mkopo kabla ya june 2024 na utatumiwa kwa ajili ya kuanza kulipa mkopo wa Eurobond.

Forum

XS
SM
MD
LG