Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 13:15

Kenya yasema haina nia ya kufunga mtandao wa Facebook


Facebook

Kenya imesema haina nia ya kuifunga mtandao wa Facebook, ambao unamilikiwa na kampuni ya Meta, waziri wake wa ICT alisema Jumatatu baada ya shirika la kuangalia uwiano wa kitaifa kutoa siku saba kwa mtandao huo kufuata sheria za matamshi ya chuki la sivyo kusimamishwa.

Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) Ijumaa ilishutumu Facebook kwa kukiuka katiba na sheria za Kenya kwa kushindwa kukabiliana na matamshi ya chuki na uchochezi jukwaani kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

"Hatuna mpango wa kufunga mtandao wowote kati ya hii” Joe Mucheru, waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia aliambia Reuters. "Uhuru wa vyombo vya habari ni jambo tunalothamini, iwe ni vyombo vya habari vya kawaifa au mitandao ya kijamii."

Kauli yake iliangazia ile ya waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang’i aliyeshutumu NCIC kwa kufanya maamuzi ya kiholela mwishoni mwa juma na kuapa kuwa jukwaa hilo halitafungwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG