Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 03:45

Kenya yapiga hatua muhimu kuelekea kupata mkopo wa IMF


Makao makuu ya Shirika la Fedha Diniani (IMF) mjini Washington.
Makao makuu ya Shirika la Fedha Diniani (IMF) mjini Washington.

Halmashauri ya Utendaji ya Shirika la Fedha Duniani, IMF imeidhinisha tathmini ya 7 na ya 8 ya programu ya Kenya, hatua ambayo IMF imesema itafungua njia kuelekea kupata mkopo wa dola milioni 606.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taifa hilo la Afrika Mashariki pamoja na maafisa wa IMF walitangaza kukubaliana kuhusu tathmini ya 7 ya program ya dola bilioni 3.6 hapo Juni, lakini kukamilika kwa tathmini za mwisho kuelekea kutolewa kwa fedha hizo kulitatizwa na maandamano ya kitaifa. Zaidi ya watu 60 walikufa kwenye maandamano yaliopelekea Rais William Ruto kusitisha msuada wa fedha uliopendekeza kuongeza ushuru.

Uchumi wa Kenya hata hivyo umeendelea kubaki imara kulinganishwa na wastani wa kieneo, wakati mfumuko wa bei ukipungua, huku fedha za kigeni zikisaidia kuimarisha shilingi licha ya mazingira magumu ya kiuchumi yaliopo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi naibu wa kwanza wa IMF, Gita Gopinath, kupitia taarifa ya Jumatano.

IMF pia ilisisitiza kuwepo kwa utawala mwema na uwazi kwenye serikali ya Kenya. Msaada wa IMF ni muhimu kwa Kenya ili iweze kukabiliana na upungufu wa fedha uliopo, uliopelekewa na viwango vya juu vya riba kwenye mikopo ya nje.

Forum

XS
SM
MD
LG