Ripoti mpya ya shirika la kimataifa linalofuatilia mizozo inaionya Kenya dhidi ya kukwama nchini Somalia ambapo inasaidia kupambana na wanamgambo wa kiislam wa al-Shabab.
Shirika hilo linasema Kenya ilitoa uamuzi wa haraka kuingilia kijeshi Somalia bila kuwa na mpango mahusi wa kuondoka. Shirika hilo linaionya Kenya kwamba operesheni dhidi ya wanamgambo hao wa Somalia huenda ikachochea mzozo zaidi wa kivita , ugaidi na vita vya kuvizia msituni na hata kwenye mipaka ya nchi yake.