Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 13:52

Kenya yaombwa kukaribisha IMF ili kufanya tadhmini ya madai ya ufisadi


Pierre-Olivier Gourinchas, Mchumi mkuu wa IMF , akihutubia kikao mjini Washington. Aprili 16,2024
Pierre-Olivier Gourinchas, Mchumi mkuu wa IMF , akihutubia kikao mjini Washington. Aprili 16,2024

Washika dau wakuu kwenye Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF, wamesihi Kenya itoe ombi kwa IMF la kuchunguza madai ya ufisadi na utalawa mbaya, kama hatua  kuelekea kupata mikopo iliyokwama kufuatia kusitishwa kwa mswada wa fedha uliolenga kuongeza kodi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mkopo wa takriban dola milioni 600, chini ya mpango wa IMF, na ambao muda wake unamalizika mwaka ujao, umekwama tangu serikali ilipositisha mpango wa kukusanya dola bilioni 2.7 kupitia kodi, kufuatia maandamano ya kitaifa.

Maandamano hayo yalioongozwa na vijana na ambayo zaidi ya watu 50 walikufa yalifichua madai ya ufisadi, pamoja na utawal mbaya, huku vijana wakilalamika kuwa kodi zao zilitumiwa na wanasiasa kuishi maisha ya kifahari. Serikali za magharibi zimekuwa zikishinikiza tadhmini ya IMF kuhusu madai hayo.

Wizara ya fedha ya Kenya haijasema lolote kuhusiana na ripoti hiyo. Tangu 2014, IMF imefanya tadhmini kwenye mataifa 14 yakiwemo Ukraine, Cameroon na Sri Lanka.

Forum

XS
SM
MD
LG