Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:58

Kenya yakubaliwa ombi lake ICC


Uma crente na Missa de Natal  na catedral de  St. Alexander Nevski em Sofia, Bulgaria.
Uma crente na Missa de Natal  na catedral de  St. Alexander Nevski em Sofia, Bulgaria.

Ombi la serikali ya Kenya limekubaliwa kwenye mkutano wa mataifa yaliobuni mahakama ya ICC, ambao ulimalizika mjini The Hague na kujadili kuhusu kesi inayomkabithi Naibu Rais William Ruto na mwandishi Joshua Sang, kwamba sasa mahakama haina ruhusa ya kutumia ushahidi uliokanushwa au uliotolewa na watu waliokufa au mashahidi waliojiondoa kwenye kesi hiyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:05 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Uamuzi huo wa mataifa yaliyounda mahakama ya ICC ulifikiwa The Hague ambapo serikali ya Kenya iliwakilishwa na zaidi ya wabunge na maseneta 120 ikiwa ni pamoja na mabalozi wa Kenya na mawaziri watatu wa serikali.

Kabla ya mkutano huo serikali ya Kenya ilitishia kujiondoa kwenye mahakama ya ICC ikiwa ombi lake litakataliwa. Kinyume na uamuzi huo mahakama hiyo ilikuwa tayari kutumia ushahidi uliokanushwa na mashahidi wa hapo awali, ushahidi wa watu waliokufa au ushahidi wa watu waliojiondoa kwenye kesi hiyo.

Mwandishi Joshua Arap Sang, December 16, 2010
Mwandishi Joshua Arap Sang, December 16, 2010

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Fatou Bensuda alikuwa amepewa ruhusa na majaji wa ICC kutumia ushahidi huo dhidi ya Ruto na Joshua Sang. Kenya ilipinga vikali uamuzi huo wa majaji. Badhi ya mataifa ya Afrika yalithitisha kujiondoa kwenye ICC ikiwa uamuzi huo utatekelezwa. Naibu wa Rais William Ruto na mwandishi Joshua wameshtakiwa katika mahakama ya ICC kwa makosa ya jinai wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 lakini wote wamekanusha mashtaka hayo.

Vyanzo vya karibu na Naibu Rais, Willian Ruto walikuwa na wasiwasi huenda mahakama ya ICC ikamtia hatiani bwana Ruto ikiwa itaruhusiwa kutumia ushahidi huo dhidi yake.

Pia Rais Kenyatta, yeye binafsi amekuwa mstari wa mbele kumtetea bwana Ruto katika kesi hiyo.

XS
SM
MD
LG