Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:06

Kenya yajaribu kupunguza ajali za barabarani


Ajali ya basi iliyotokea kusini magharibi ya Kenya, watu 20 walifariki katika ajali hiyo.
Ajali ya basi iliyotokea kusini magharibi ya Kenya, watu 20 walifariki katika ajali hiyo.

Msako wa magari mabovu ya huduma za umaa katika lengo la kupunguza ajali za barabarani umezusha mgomo wa matatu katika baadhi ya miji ya Kenya

Rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga wa Kenya wamekitaka kikosi cha polisi wa usalama wa barabarani kufanya msako wa kuondoa barabarani magari mabovu na yale yanayokiuka sheria za barabarani, kwa lengo la kupunguza ajali za magari.

Katika muda wa siku tatu wiki hii, ajali mbili za barabarani zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 20. Ajali moja iliyotokea Jumapili katika mkoa wa Mashariki, kati ya mji wa Mwingi na Garissa ilisababisha vifo vya watu 13 na ajali nyingine iliyotokea mapema Jumamosi karibu na mji wa Voi, mkoa wa Pwani takribakan kilometa 120 kutoka Mombasa.

Mwezi uliopita rais Kibaki na waziri mkuu Odinga walihudhuria maziko ya watu wengine 23 karibu na Machakos waliofariki kutokana na ajali ya basi dogo walipokuwa wanatoka katika hafla ya kupanga harusi ambapo wengi wao walikuwa ni ndugu.

Ajali hizio zimepelekea serikali ya Kenya kutangaza vita dhidi ya huduma za magari ya uchukuzi wa umma wanaokiuka sheria za barabarani.

Mwenyekiti wa bodi ya kutoa leseni Hassan Ole Kamaro amewalaumu wamiliki wa baadhi ya magari, lakini wamiliki kwa upande wao wameikosoa bodi hiyo pamoja na polisi wa usalama barabarani wanaoendesha msako huo.

Hayo yote yalipelekea mgomo wa wamiliki wa magari ya usafiri maarufu kama matatu kutokana na magari kufichwa magari hayo na kupelekea wafanyabiashara wengi kupata hasara kwa biashara katika mji wa Mombasa.

Msako huo hivi sasa umeanza katika mji wa Machakos na unatazamiwa kuendelea katika mji mkuu wa Nairobi.

XS
SM
MD
LG