Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 02:35

Kenya yaimarisha ulinzi sherehe za kuapishwa Kenyatta


Uhuru Kenyatta
Uhuru Kenyatta

Matayarisho ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne yamekamilika na tayari vyombo vya usalama vimeimarisha ulinzi wa kutosha kwa wale watakao hudhuria sherehe hizo, kamati ya maandalizi imesema.

Sherehe hizo zitagharimu kiasi cha shilingi milioni 300, na habari za ndani zinasema kuwa kiwango kikubwa cha fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ulinzi.

Mnamo mwaka 2013, wakati Rais Kenyatta alipokuwa anaapishwa kwa awamu ya kwanza, kamati hiyo ilikuwa inahitaji shilingi bilioni 1.2, ambazo ofisi ya Hazina baadae ilipunguza kiwango hicho kufikia shilingi milioni 374, na shilingi milioni 64 zilitolewa na Mahakama.

Katika bajeti ya mwaka 2017, hazina imetoa shilingi milioni 384 kwa ajili ya sherehe hizo, ambazo ni shilingi milioni 10 zaidi kuliko ilivyokuwa 2013.

Siku ya Ijumaa, kamati hiyo, inayoongozwa na mkuu wa wafanyakazi wa ikulu na mkuu wa wafanyakazi wa Umma, Joseph Kinyua haikutoa mchanganuo wowote wa shilingi milioni 300 vipi zitatumika. Alisema tu kiwango hicho ni cha “kati na kinatosheleza”.

Kamati ya maandalizi ya kuapishwa kwa Rais kuchukua wadhifa wake imesema kuwa imemwalika kiongozi wa Muungano wa Upinzani, Nasa, Raila Odinga na wagombea wengine sita wa kinyang’anyiro hicho cha urais, pamoja na wagombea wenza wao.

Kinyua pia amemtaka Odinga kusitisha mpango wa maandamano ya Nasa uliopangwa siku ya Jumanne.

Ni lazima sote tushikamane katika kujenga umoja wa taifa la Kenya,” amesema Kinyua kuwaambia waandishi wa habari katika kituo cha kimataifa cha michezo cha Moi, Kasarani, ambapo rais ataapishwa hapo.

Aliendelea kusema kuwa: “Tukio la kuapishwa Rais siku ya Jumanne ni la kihistoria.

XS
SM
MD
LG