Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 18:53

Kenya yaahidi kuvamia vituo vya wanamgambo kote Somalia


Wapiganaji wa Al- shaabab wakionesha silaha kusini mwa Mogadishu
Wapiganaji wa Al- shaabab wakionesha silaha kusini mwa Mogadishu

jeshi la Kenya limesema litavamia vituo vya wanamgambo kote nchini somalia

Wasomali wanajiandaa wenyewe na mashambulizi ya anga kutoka jeshi la Kenya baada ya msemaji wa jeshi Emmanuel Chirchir kuonya kuwa Kenya ina mpango wa kuvamia vituo vya wanagambo kote Somalia.

Chirchir amesema ndege za jeshi la Kenya zina tarajia kusaka silaha ambazo zilisafirishwa kuingia Somalia kwa kutumia ndege mbili na kupewa kundi la wanamgambo la al- Shabab .

Amewasihi wasomali kuwa makini juu ya mashambulizi hayo. Jeshi la Kenya lilisema jumanne kwamba lina taarifa za uhakika kwamba ndege hizo zilitua kusini mwa mji wa Baidoa nchini Somalia zikiwa zimebeba silaha zilizokuwa zinapelekwa kwa al- shabab .

Ingawa Chirichir hakusema ndege hizo zilikuwa zinatoka wapi lakini vyombo vya habari vya ndani vinailaumu Eritrea.

XS
SM
MD
LG