Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 08:17

Wanaharakati Kenya waghadhibishwa kutopitishwa kwa mswaada wa jinsia


Wabunge Millie Adhiambo (kushoto) and Florence Mutua (kulia) wakiondoka bungeni wakati wa hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta kuhusu hali ya kitaifa March 2016.

Wanaharakati wa kutetea maswala ya usawa wa jinsia humu Kenya wameelezea hofu yao kuhusu msukosuko wa kikatiba unaokodolea macho taifa hilo baada ya bunge kushindwa kuidhnisha mswaada wa sheria kuhusu theluthi mbili ya uwakilishi wa jinsia.

Kwa mujibu wa tume ya kitaifa kuhusu usawa wa jinsia Kenya, mswaada huo ambao ulipaswa kuidhinishwa kufikia tarehe 27 mwezi Agosti mwaka jana unapaswa uwe sheria kwa kuzingatia vipengele vya 27 sehemu ya 8 na 82 sehemu ya (B) vya katiba kuhusu uwakilishi wa kijinsia kwenye nyadhifa za kuchaguliwa nchini humo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:19 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mswaada huo ulilenga kusawazisha muundo wa nyadhifa za uteuzi humu nchini kwa kutoruhusu jinsia moja kuwa na zaidi ya theluthi mbili katika nafasi za uchaguzi.

Kwa sasa viongozi wa wanawake pamoja na tume ya taifa kuhusu usawa wa jinsia wanawahimiza wakenya kuwapigia kura wanawake watakaojitosa katika nafasi za ubunge kama njia ya kuwaadhibu wabunge wanaume wanaopinga sheria hiyo ya kikatiba.

Uwakilishi wa wanawake katika siasa kwa sasa ni asilimia 15 ikilinganishwa na asilimia 56 nchini Rwanda , asilimia 42 afrika kusini , asilimia 36 nchini tanzania na asilimia 35 Uganda. Japo asilimia 15 ni hatua nzuri baada ya bunge la kumi kuwa na asilimia 9.4 bado ni chache mno hasa kwa wakati huu ambapo ushiriki wa wanawake katika siasa umeboreka katika mataifa mengi ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG