Serikali ya Kenya sasa inaonekana kutekeleza sheria mpya ya kuwaadhibu
magaidi, kama ilivyopitishwa katika marekebisho ya sheria kuhusu
usalama wa taifa hilo la Afrika Mashariki.
Katika kisa cha hivi punde (Alhamisi) mahakama kuu mjini Mombasa
imetoa hukumu ya kifo kwa mshukiwa wa ugaidi, Thabit Yahya, aliyeshtakiwa
miaka minne iliyopita kwa kulipua mgahawa mmoja ambapo mtu mmoja
aliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
VOA ilikuwa ya kwanza kutangaza kuhusu shambulizi hilo lililotokea mwezi Mei mwaka wa 2012 wakati wa usiku katika mgahawa uliojulikana kama Bella Vista ambapo watu wengi walijeruhiwa, wakati washambuliaji walipotumia maguruneti kutekeleza kitendo hicho.