Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:28

Waalimu warejea madarasani Kenya


Wanafunzi wakijisomea wakati wa mgomo katika shule ya msingi Nairobi, September 9, 2015.
Wanafunzi wakijisomea wakati wa mgomo katika shule ya msingi Nairobi, September 9, 2015.

Waalimu wamerejea madarasani nchini Kenya leo huku kukiwa na maoni tofauti nchini baada ya chama cha waalimu kumaliza mgomo uliochukua karibu wiki tano.

Waalimu warejea madarasani Kenya
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kulingana na viongozi wa chama cha waalimu wamemaliza mgomo huo kwa shingo upande kwa sababu ya amri ya mahakama na kutaka kupata ridhaa na serikali.

Chama cha elimu kinasema kitaendelea kupambana mahakamani mpaka haki za waalimu zimepatikana.

Mwandishi wetu ametembelea shule kadha mjini Nairobi na kushuhudia wanafunzi wengi wakiwa wamerejea madarasani baada ya kukaa nyumbani kwa wiki tano bila masomo.

XS
SM
MD
LG