Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 09:59

Kenya yawafukuza waalimu kwa kuharibu watoto

Mwanafunzi wa shule moja Kenya akifanya uchoraji.

Maafisa wa Kenya wanasema zaidi ya waalimu 1,000 wamefukuzwa kazi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kwa sababu ya kufanya mapenzi na wasichana wanafunzi.

Maafisa wa Kenya wanasema zaidi ya waalimu 1,000 wamefukuzwa kazi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kwa sababu ya kufanya mapenzi na wasichana wanafunzi.

Maafisa wa elimu wanasema waalimu hao wamefukuzwa kwa kuwapa mimba wanafunzi wa shule na vitendo vingine vya ngono. Matukio mengi yamefanyika katika shule za msingi za umma.

Pamoja na kufukuzwa kazi, baadhi ya waalimu wanakabiliwa na mashitaka ya jinai katika mahakama.
Maafisa wanasema zaidi ya waalimu 500 wamefukuzwa kazi mwaka huu kwa kuhusika na unyanyasaji wa ngono na kwamba waalimu 600 waliachishwa kazi mwaka jana.

XS
SM
MD
LG