Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 15:57

Kenya kubadilisha makamishna wa tume ya uchaguzi


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Serikali yake ilitrangaza tarehe 27 mwezi Septemba mwaka wa 2016 kuwa imechukua hatua za kubadilisha makamishna wa tume ya uchaguzi

Serikali ya Kenya imesema leo kwamba inachukua hatua za kubadilisha makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini humo, IEBC, ikiwa ni kuambatana na mojawapo ya makubaliano kati yake na upinzani, ya kumaliza mzozo uliopelekea maandamano na vurugu mapema mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taarifa iliyotolewa na serikali hii leo, imesema kuwa kamati iliyobuniwa na iliyo na wawakilishi kutoka kwa mashirika kadhaa ya kiserikali, itaongoza majadiliano yatakayopelekea kuondoka kwa makamishna wa tume hiyo, bila ya ubishi wala Malalamishi yoyote.

Pande mbili zilizokuwa zikizozana, hatimaye zilifanya mazungumzo katik majengo ya bunge la nchi hiyo, kutafuta mbinu za kumaliza mgogoro huo wa kisiasa, huku upinzani ukiendelea kushinikiza tume hiyo kuondoka na ukishikilia kwamba haifai kuratibu wala kusimamia uchaguzi, ambao umepangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka ujao.

XS
SM
MD
LG