Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:28

Kenya yafunga uchunguzi wa meli iliyokutwa na silaha


Moja kati ya meli nyingi ambazo hutia nanga bandari ya Mombasa.
Moja kati ya meli nyingi ambazo hutia nanga bandari ya Mombasa.

Polisi nchini Kenya imekamilisha uchunguzi kuhusu shehena ya silaha iliyokutwa katika meli moja iliyosajiliwa Norway katika bandari ya Mombasa.

Inspekta Mkuu wa polisi wa Kenya, Joseph Boinnet, amesema sasa shehena hiyo inaweza kusafirishwa DRC ambako ilikuwa inaelekea kwa majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.

Meli hiyo ilizuiliwa katika bandari ya Mombasa Septemba 17 baada ya kukutwa na shehena hiyo ya silaha na uchunguzi kuanza mara moja. Taarifa zimethibitsha kwamba uchunguzi ulifungwa rasmi Ijumaa na wafanyakazi wa meli hiyo wakaruhusiwa kurudi makwao.

Mamlaka ya Bandari ya Mombasa imethibitishia vyombo vya habari Kenya kwamba uchunguzi wa meli hiyo umemalizika na shehena imeachiliwa ipelekwe DRC.

Meli hiyo MV Hoeg Transporter iliondoka katika bandari ya Mombasa Septemba 25 na kuendelea na safari yake.

XS
SM
MD
LG