Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:56

Seneta wa Kenya ahudhuria Kongamano Marekani kupinga ugaidi


Senata Lenny Kivuti akizungumza mbele ya jengo la bunge Washington DC pembeni ya mbunge wa Marekani Frederica S.Wilson wa Florida.
Senata Lenny Kivuti akizungumza mbele ya jengo la bunge Washington DC pembeni ya mbunge wa Marekani Frederica S.Wilson wa Florida.

Seneta Lenny Kivuti, alitoa wito kwa mataifa yaliyoendelea kuyasaidia kimikakati mataifa ya Afrika yanayokumbwa na changamoto nyingi wakati yanapokabiliana na jinamizi la ugaidi.

Na BMJ Muriithi

Seneta wa Kaunti ya Embu, Kenya, Bw Lenny Kivuti, siku ya Alhamisi alitoa wito kwa mataifa yaliyoendelea kuyasaidia kimikakati mataifa ya Afrika yanayokumbwa na changamoto kubwa wakati yanapokabiliana na jinamizi la ugaidi.

Kivuti alikuwa akizungumza katika majengo ya bunge la Marekani alipohudhuria hafla ya kuadhimisha miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana 276 kutoka kwa shule moja katika mji wa Chibok, nchini Nigeria.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mamia ya watu, wakiwemo wanaharakati wa kampeni ya kimataifa ya ‘Bring Back Our Girls’ yaani Turudishieni wasichana wetu, ambao waliongozwa na Bi Frederica Wilson, mwakilishi wa eneo la 24 katika jimbo la Florida kwenye bunge la Marekani. Maadhimisho mengine kama hayo yalifanyika katika miji tofauti tofauti ulimwenguni kote siku hiyo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika muda mfupi baada ya hafla hiyo, seneta Kivuti alisema kundi la Boko Haram linawiana kwa njia nyingi na lile la Al-Shabaab ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi yaliyokithiri katika eneo la Afrika Mashariki na kupelekea umwagikaji wa damu hususan katika nchi ya Kenya.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:45 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

“Ni sharti Afrika ishikane pamoja ili mataifa yaliyoendelea yaone kwamba hata kama tunaomba usaidizi, sisi wenyewe tuna azima ya kupambana vilivyo na jinamizi hili,” alisema Kivuti.

“Tunaweza kuyaangamiza makundi haya iwapo mataifa kama Marekani yatatusaidia kiteknolojia kwani mbinu nyingi zinazotumiwa nao zilifumbuliwa hapa hapa Marekani. Mimi sioni kama ni sawa kwa serikali kufanya mazungumzo na magaidi kwa sababu hawana nia njema hata kidogo,” aliongeza Kivuti.

Kenyan Senator Lenny Kivuti chats with a Congresswoman at the Capitol in Washington DC.
Kenyan Senator Lenny Kivuti chats with a Congresswoman at the Capitol in Washington DC.

Seneta huyo alitoa mchango wa $2,000 kuwasaidia wasichana wanne ambao ni baadhi ya waliotoroka kutoka kwa utekaji huo wa Boko Haram, na ambao wamepata nafasi za kuendelea na Masomo nchini Marekani.

Wasichana hao wa Chibok walitekwa nyara usiku wa kuamkia Aprili 14, 2014. Ingawa baadhi yao walifanikiwa kutoroka, 219 bado hawajulikani waliko. Tukio hilo lilipelekea kampeni ya kimataifa kuwataka wasichana hao warejeshwe, na ambayo imeungwa mkono na wengi ulimwenguni kote, wakiwemo watu mashughuri ambao ni pamoja na wajumbe kadhaa wa bunge la Marekani na mke wa rais, Michelle Obama.

Familia za wasichana ambao bado hawajapatikana zinaendelea kuwasihi magaidi wa Boko haram kuwaachilia huru ili waendelee na masomo yao.

Kenyan Senator Lanny Kivuti (Center) at Capitol Hill
Kenyan Senator Lanny Kivuti (Center) at Capitol Hill

Siku ya Alhamisi watu wa tabaka mbali mbali walionekana wakibeba mabango yenye maandishi "Warejesheni wasichana wetu," na kufanya maandamano ya amani.

Maadhimisho hayo yalifanyika siku ambayo kituo cha televisheni cha CNN kilionyesha video inayoaminika kuwa ya wasichana haoa ambao walionekana kuvaa hijabu za kiislamu. Mama mmoja alionekana akimtambua binti yake kwenye tarakilishi na kuangua kilio akisema “Saratu wangu”.

Tazama video hapa:

XS
SM
MD
LG