Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 22:38

Afisa wa Kenya arejeshwa kutoka Olimpiki


Wanariadha wa Kenya waliandamana mbele ya makao makuu ya Athletics Kenya mwaka huu

Kenya imemwamuru kurudi nyumbani kutoka katika michezo ya Olimpiki Rio de Janeiro, Brazil afisa mmoja wa timu ya riadha kufuatia madai kuwa aliahidi kuwalinda wanariadha wasifanyiwe vipimo vya dawa za kuongeza nguvu.

Afisa huyo Michael Rotich inadaiwa alikuwa anaomba rushwa ya dolla elfu 13 kutoka kwa wanariadha ili aweza kuwapa taarifa za mapema endapo maafisa wanaopima matumizi ya dawa wanakuja kuwapima.

Wanariadha wa Kenya katika mazoezi magharibi mwa Kenya
Wanariadha wa Kenya katika mazoezi magharibi mwa Kenya

Gazeti la Sunday Times la London liliripoti kuwa afisa huyo wa riadha wa Kenya alichukuliwa video ya siri akiahidi kuwalinda wanaridha katika upimaji huo kwa kuwapa taarifa za mapema.

Madai hayo ni pigo jingine kwa sifa za riadha Kenya baada ya madai ya utumiaji dawa za kuongeza nguvu katika miezi ya karibuni.

Mwandishi mmoja wa Kijerumani aliripoti kuwa chama cha riadha Kenya - Athletics Kenya - kimesema Rotich anarudishwa nyumbani kupisha uchunguzi katika swala hilo.

Taarifa hiyo pia imesema kuwa huenda kesi hiyo ikafikishwa kwa polisi wa Kenya kwa uchunguzi zaidi na hatua za kisheria..

XS
SM
MD
LG