Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 16:11

Raila Odinga 'kuapishwa' Januari 30?


Raila Odinga apiga kura Kibra, Agosti 8, 2017.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesisitiza kuwa ataapishwa, kutwaa madaraka na kuunda baraza lake la mawaziri hata kama ikimlazimu kufanya hivyo akiwa mafichoni.

Katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, Bw. Odinga amefuta uwezekano wa kufanya mazungumzo na rais aliyepo mamlakani Uhuru Kenyatta ili kuweza kupatikana kwa suluhu ya kisiasa kati ya wawili hao.

Bw. Odinga amesema kuapishwa kwake kutafanyika Januari 30 kama ilivyopangwa awali na kila mkenya amealikwa kuhudhuria hafla hiyo na kueleza kuwa huenda ikamlazimu afanye hivyo akiwa mafichoni.

Rais Kenyatta kwa upande wake amekuwa akiuhimiza upinzani wa NASA kuachana na siasa kwani kipindi cha siasa tayari kimekamilika kwa mujibu wa kalenda ya matukio nchini Kenya.

Matamshi ya Bw. Odinga kuwa ataapishwa na kuwa rais wa wananchi yamekuwa yakiibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya wengi wakijiuliza kule anapoelekea kutekeleza majukumu ya urais wakati ikulu ya Kenya ina mwenyeji ambaye ni Uhuru Kenyatta, Odinga hakubaliani na hilo.

Wachambuzi wa siasa za Kenya wamekuwa wakitofautiana kwa kauli kuwa huenda Odinga na vinara wenzake wanatumia kisingizio cha kuapishwa kama chambo cha kutaka mazungumzo na Bw. Kenyatta na vile vile kujumuishwa katika serikali, lakini Bw. Odinga anasema hilo si kweli hata kidogo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG