Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 11:48

Kenya na India waahidi kuimarisha uhusiano wa nchi zao


Waziri Mkuu wa Kenya, Narendra Modi (L) na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Julai 11, 2016

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi na Rais wa kenya Uhuru Kenyatta, walihutubia kikao cha waandishi wa habari mjini Nairobi Jumatatu alasiri na kuahidi kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili huku kiongozi huyo akiwa katika siku yake ya mwisho ya ziara yake barani Afrika.

Mapema Jumatatu Modi alfanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Nairobi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Ikulu, Manoah Esipisu, viongozi hao walitia saini makubaliano kuhusu uimarishaji wa sekta za biashara, afya, mawasiliano, usalama, utalii na kilimo.

Modi aliwasili nchini Kenya Jumapili, baada ya kufanya ziara kama hiyo nchini Tanzania. Kiongozi huyo anaandamana na ujumbe wa zaidi ya watu themanini, wakiwemo wafanyabiashara kutoka India.

Kabla ya kuondoka, Modi anatarajiwa kutembelea ofisi za Umoja wa Mataifa katika eneo la Gigiri kabla ya kuelekea katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Ziara yake nchini Kenya inakamilisha safari yake ya mataifa manne barani Afrika.

Tayari ameshatembelea nchi ya Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini.
Narendra Modi amekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa India kuwahi kuzuru Kenya baada ya kipindi cha miaka 35.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG