Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:38

Kenya: Mudavadi ajiunga na chama cha UDFP


Musalia Mudavadi (kati kati) akitangaza kujiuzulu kwake kutoka ODM akiwa pamoja na Najib Balala (kulia)
Musalia Mudavadi (kati kati) akitangaza kujiuzulu kwake kutoka ODM akiwa pamoja na Najib Balala (kulia)

Musalia Mudavadi ajiuzulu wadhifa wa waziri wa serikali za majimbo na kujiunga na chama kipya cha UDPF.

Naibu waziri mkuu wa Kenya Bw. Mudavadi alijiuzulu kama naibu mwenyekiti wa chama cha ODM na kutangaza kujiunga na chama kipya cha United Democratic Forum Party, UDFP.

Katika sherehe za kukitangaza chama kipya katika ukumbi wa jengo la Kenyatta International Conference Center mjini Nairobi siku ya Jumanne, Bw Mudavadi alisema ameamua kujiunga na chama na watu wenye dhamira ya kuheshimu utawala wa sheria na muongozo wa kuleta mabadiliko ya kweli.

Akizungumza na Sauti ya Amerika waziri wa zamani wa utali wa Kenya Najib Balala aliyehudhuria sherehe hizo alisema, uwamuzi wa Mudavadi ni hatua ya busara kuweza kuungana na watu wenye nia ya kuleta mageuzi ya kidemokrasia na manedeleo ya kweli nchini Kenya.

Bw. Balala alisema yeye si moja wapo wa wanachama wa chama hicho kinacho waleta pamoja wanasiasa walojiondowa hivi karibuni na chama cha ODM lakini alisema ana nia ya kutangaza chama chake binafsi wiki moja ijayo na anahakika vyama vyenye mawazo ya sawa vitaungana kumchangua mgombea moja kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

XS
SM
MD
LG