Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 16:31

Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya afutwa kazi


Waziri Joseph Ole Lenku mjini, Nairobi, 2013.
Waziri Joseph Ole Lenku mjini, Nairobi, 2013.

Waziri wa usalama wa taifa nchini Kenya Joseph ole-Lenku amefukuzwa kazi wakati Mkuu wa Majeshi ya Polisi David Kimaiyo amejiuzulu kufuatia mauaji mengine ya watu 36 Jumatatu usiku katika county ya Mandera nchini humo.

Kundi la kigaidi la al-Shabab limedai kuhusika katika mauaji hayo ya Jumatatu usiku katika mgodi wa kuchimba mawe nje kidogo ya mji wa Mandera.

Ripoti zinasema washambuliaji walivamia kambi ya wafanyakazi katika mgodi huo na kuwapanga msitari na kuwapiga risasi na wengine kuuawa kwa mapanga. Ripoti zaidi zinasema washambuliaji hao walichagua wakristo na kuwauwa na kuwaacha waislamu.

Rais Uhuru Kenyatta amelihutubia taifa leo akiahidi jitihada zaidi kupambana na magaidi na kuboresha hali ya usalama nchini humo.

Mauaji haya mapya yamekuja wiki moja tu baada ya mauaji mengine ya watu 28 waliokuwa wakisafiri katika bus kutoka Mandera kuelekea Nairobi.

XS
SM
MD
LG