Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 16, 2024 Local time: 14:12

Kenya:mafuriko yaua watu 42 baada ya bwawa kupasuka


Wakazi wa kitongoji cha Mathare wakisimama karibu na nyumba zilizoharibiwa na mafuriko, kufuatia mvua kubwa mjini Nairobi, Aprili 24. Picha ya AFP
Wakazi wa kitongoji cha Mathare wakisimama karibu na nyumba zilizoharibiwa na mafuriko, kufuatia mvua kubwa mjini Nairobi, Aprili 24. Picha ya AFP

Watu 42 wamefariki katika mafuriko katika eneo la Mai Mahiu katikati mwa Kenya baada ya bwawa kupasuka mapema Jumatatu, na idadi ya vifo inaweza kuongezeka, polisi wamesema.

Picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya X na vyombo vya habari vya Kenya, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na mamlaka ya barabara kuu zimeonyesha matukio ya baada ya mafuriko, miti iliyokatika na gari moja lililokwama kwenye magogo na matope.

“Kufikia sasa, tumefanikiwa kupata miili 42, ikiwemo miili ya watoto 17, kufuatia tukio la asubuhi ambapo bwawa lilipasua kingo zake eneo la Kijabe na shughuli za uokoaji na utafutaji zinaendelea,” kamanda wa polisi wa Naivasha Stephen Kirui amewambia waandishi wa habari kwenye eneo la uokoaji.

Mapema Jumatatu, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema liliwapeleka watu kadhaa kwenye kituo cha afya huko Mai Mahiu kutokana na mafuriko.

Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa na mafuriko tangu mwezi uliopita imefikia zaidi ya 140.

Forum

XS
SM
MD
LG