Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 18:05

Kenya kufanya mazishi ya kitaifa ya Mwai Kibaki wiki ijayo


Hayati Rais wa tatau wa Kenya Mwai Kibaki.

Kenya itafanya mazishi ya kitaifa wiki ijayo ya rais wa zamani Mwai Kibaki, ambaye aliliongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa zaidi ya muongo mmoja, Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiangi alisema Jumamosi.

Kibaki, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 90, alihudumu kama rais wa tatu wa nchi hiyo kuanzia Desemba 2002 hadi Aprili 2013, akichukua hatamu kutoka kwa utawala wa kimabavu wa Daniel arap Moi.

“Mkuu huyo wa zamani wa nchi atapewa mazishi ya kiserikali kwa heshima ya hali ya juu kwa sababu ya utumishi wa kipekee alioutoa kwa nchi yetu," Matiangi alisema.

Kibaki, ambaye maisha yake ya kisiasa yalianza tangu kuzaliwa kwa Kenya huru, atazikwa Jumamosi ijayo nyumbani kwake Othaya katika nyanda za juu za Nyeri, alisema.

XS
SM
MD
LG