Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:35

Kenya kuendeleza marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki kuokoa mazingira


Mtoto amevaa taka ya chupa za plastiki zinazotolewa na waharakati wa mabadiliko ya mazingira siku ya kimataifa ya kuchukua hatua kulinda hali ya hewa chini ya kauli mbiu ''#AfricaIsNotADumpster'' (Afika sio jalala) katika viwanja vya Uhuru Park's Freedom Corner, Nairobi, Kenya.

Siku ya Jumatatu June 5, ni siku ya mazingira duniani, lakini changamoto kuu inaendelea kua ni uchafuzi unaotokana bidhaa za plastic.

Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira, UNEP zinaonyesha kuwa takriban tani million 430 za uchafu wa plastiki huzalishwa kila mwaka.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya mataifa ya Afrika ikiwemo Kenya yanaendeleza marufuku ya matumizi wa mifuko ya plastic.

Hata hivyo utafiti unaonyesha bado kuna changamoto za bidhaa za plastic zisizoweza kuchakatuliwa.

Mashirika ya serikali na asasi za kiraia Kenya yameungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya mazingira duniani.

Washirika hao wameshiriki katika kusafisha miji, vituo vya afya na mitaa ya mabanda kama njia ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa mazingira safi.

Licha ya Kenya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastic miaka 7 iliyopita , hili halijatatua changamoto ya kumaliza uchafuzi wa taka za plastic.

Mamlaka ya kitaifa inayoshughulikia mazingira, inashikilia kuwa asilimia 80 ya wakenya wanatekeleza sheria hii japo kuna changamoto ya mifuko ya plastic kutoka mataifa ya nje.

Mwaka 2030, Kenya ina mikakati ya kuchakata bidhaa za plastic ili kupunguza utupaji ovyo wa taka hizo za plastic.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Nema, Programu hii, kwa lugha ya kimombo, Circula Economy ni suluhu kwa uchafuzi wa plastic ambazo zimekuwa sio tu hatari kwa mazingira bali pia afya hasa nyakati za mvua.

Wanaharakati wa mazingira wanashikilia kuwa Kenya ina sheria muafaka za kudhibiti uchafuzi wa plastic kwa kutilia mkazo utekelezaji wake na pia kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa mazingira safi.

Ripoti ya shirika la mazingira la umoja wa mataifa, UNEP, uchafuzi wa plastic unaweza kupunguzwa kwa asilimia 80 kufikia mwaka 2040 iwapo nchi na kampuni zinweza kuweka sera thamiti mabadiliko ya masoko kwa kutumia teknolohia iliopo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Amina Chombo, Kenya

Forum

XS
SM
MD
LG