Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 25, 2023 Local time: 17:03

Kenya itaendelea kupambana na al-Shabaab Somalia


Jenerali Julius Karangi, mkuu wa majeshi ya Kenya akizungumza na waandishi habari Oktoba 29, 2011

Mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Julius Karangi asema hakuna muda maalum uliotengwa kuondoka Somalia

Wizara ya Ulinzi ya Kenya imesema haijatenga muda wa kumaliza operesheni zake dhidi ya wanamgambo wa al-Shabaab nchini Somalia. Wizara hiyo imesema majeshi yake yataondoka Somalia pale tu yatakapohakikisha Wakenya wako salama. Maafisa wa Kenya wamesisitiza kwamba hawako vitani na taifa la Somalia lakini wako katika vita dhidi ya wanamgambo wa al-Shabaab.Mkuu wa majeshi huko Kenya Jenerali Julius Karangi aliwaambia waandishi habari Jumamosi kuwa kampeni dhidi ya al-Shabaab nchini Somalia haijatengewa muda wa kumalizika na kwamba maamuzi hayo yamo mikononi mwa Wakenya pale watakapohisi wako salama hasa kwenye mipaka yake.Jeshi la Kenya limesema limeuwa mamia ya wanamgambo wa al-Shabaab katika muda wa siku 15 tangu ilipowavamia wanamgambo hao wa Somalia na kwamba mwanajeshi wake mmoja ameuwa katika mapigano hayo. Wanajeshi watatu wa Kenya pia hawajulikani waliko, wawili walitekwa nyara mapema mwaka huu na wa tatu alitoweka katika bahari ya Hindi akiwa katika harakati za kumwokoa mwanamke raia wa Ufaransa aliyetekwa nyara. Jenerali Karangi amesisitiza kuwa uvamizi wa majeshi ya Kenya dhidi ya wanamgambo wa al-Shabaab huko Somalia ulitokana na visa vya utekaji nyara na mashambulizi mengine ndani ya Kenya.

XS
SM
MD
LG