Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:37

Je, Kenya itaweza kuendesha reli mpya kwa faida?


Rais Uhuru Kenyatta, watatu kushoto akiangalia treni ya mizigo ikianza safari zake kutoka Mombasa, Kenya Mei 30, 2017.
Rais Uhuru Kenyatta, watatu kushoto akiangalia treni ya mizigo ikianza safari zake kutoka Mombasa, Kenya Mei 30, 2017.

Kuna utani unaendelea kuenea baada ya kuzinduliwa kwa reli ya Standard Gauge ya mabilioni ya fedha mwezi Juni 1, ukibeza kuwa safari ya kwenda bichi ni mwendo wa masaa manne kutoka eneo la Syokimau, ilioko pembezoni wa mji wa Nairobi, Kenya.

Lakini kwa muono wa wataalamu wa uchumi na sera ya umma waliokutana Nairobi Jumamosi, utabiri ulikuwa machozi yataanza kutiririka kipindi kifupi tu pale ambapo itakuja kubainika kuwa hakukuwa na mkakati wa kibiashara.

Madai ni kuwa mkopo huu wenye gharama kubwa—uliotolewa katika sarafu ya dola na mabenki ya China—na kutumika kujengea reli hiyo ni lazima uanze kulipwa kuanzia mwaka 2019.

Wakati dola zilizotolewa na bank ya China ya Export-Import bank zikibadilishwa katika shilingi za Kenya katika thamani ya dola ya hivi sasa na kuongezwa katika kile ambacho serikali imekiongezea katika mradi huo, gharama kamili ya ujenzi iliyotolewa na ofisi ya Hazina ya taifa imeonyesha kufikia shilingi bilioni 425.9. Na pindi unapoongeza faida ya benki, inafikia karibu na shilingi bilioni 500.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vinasema ukweli ni kuwa Kenya ilikopa dola bilioni 3.23. Kwa kiwango cha thamani ya dola hivi leo, hiyo ni sawa na Sh bilioni 332,7. Angalau dola bilioni 1.6 (Sh bilioni 164.8) zilitolewa kama mkopo hafifu ambao utalipwa kwa miaka 20, baada ya kupewa mapumziko ya kutochelewa kulipa kwa miaka saba.

Kenya imekuwa ikilipa sh bilioni 1.6 (dola milioni 16) kila baada ya miezi sita na faida juu tangu mwaka 2014 wakati pesa hizo zilipotolewa.

Wakati malipo ya mkopo wenyewe yakianza mwaka 2021, nchi hiyo itakuwa inalipa sh bilioni 14 kila mwaka kwa kipindi cha miaka 13 mpaka mwaka 2034.

Wataalamu hao wanadai kuwa ushindi wa Jubilee ambao sasa wanaufurahia kutokana na treni hiyo ya abiria itakayo safari kati ya Mombasa na Nairobi ni kuwa wakati wa pendekezo la kujenga reli hiyo, ahadi ilikuwa itakuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo mizito ambayo ingewezesha reli hiyo kujiendesha yenyewe.

Hivi sasa imekamilika, na wakati wa kuanza kulipa deni umekaribia, lakini upande wa operesheni za kibiashara unabakia na maswali mengi.

“Sisitizo jipya… ni kuwa sasa tunaweza kwenda Mombasa kwa masaa manne. Inakuwa kama vile hiyo ndio ilikuwa sababu ya msingi kwa nchi kupoteza fedha chungu nzima kwa ajili ya ujenzi wa reli.

Hoja ya awali ilikuwa tunahitaji kufikisha mizigo kwa kuacha kutumia barabara na hivyo kusafirisha kwa reli,” amesema Kiriro wa Ngugi, ambaye ni mtaalamu wa sera ya umma.

XS
SM
MD
LG