Upatikanaji viungo

Viongozi wachukua misimamo tofauti kuhusu Tume ya Uchaguzi, Kenya


Polisi wa kutuliza ghasia wakati wa maandamano ya wafuasi wa CORD, Jumatatu, Nairobi

Viongozi kutoka mirengo tofauti ya kisiasa nchini Kenya wameendelea kutofautiana kuhusu kuvunjwa kwa Tume ya Uchaguzi swala ambalo limepelekea maandamano ya mara kwa mara kutoka kwa vyama vya upinzani hasa kwenye mji mkuu, Nairobi.

Kutokana na shinikizo linaloendelea nchini Kenya kutoka kwa muungano wa vyama vya upinzani, CORD la kuvunjwa kwa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka ,IEBC pamoja na maandamano ambayo yamekuwa yakishuhudiwa, Harrison Kamau wa VOA aliweza kuzungumza na Dkt Naomi Shaban ambae ni Mbunge wa Taveta na anaeengemea mrengo wa Muungano wa Jubilee pamoja na wakili Paul Mwangi ambae ni mshauri wa kiongozi wa mrengo wa CORD, Raila Odinga na akawauliza misimamo yao kuhusu swala lote hilo.

Sikiliza mahojiano kwa taarifa zaidi.

XS
SM
MD
LG