Wabunge wanne kutoka mrengo wa Jubilee nchini Kenya wamewasilisha kesi Mahakamani ya kuzuiya maandamano yaliopangwa kufanyika kila wiki kwenye ofisi za Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC yakiongozwa na muungano wa vyama vya upinzani nvhini humo, CORD kwa nia ya kushinikiza kuvunjwa kwa Tume hiyo.
Kufutaia hatua hiyo,Harrison Kamau wa VOA amezungumza na wakili Agina Ojwang' kutoka Nairobi na kwanza akamuuliza iwapo kesi hiyo inahujumu haki ya uhuru wa kuandamana inayotolewa na Katiba. Kwa habari za kina, zikliza mahojiano.