Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:31

Kenya haikuhusika na mashambulio ya Afgoye Somalia


Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia
Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia

Msemaji wa jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir anasema Kenya haijahusika na mashmabulio ya Afgoye, moja ya ngome za Al-Shabab.

Akizungumza na sauti ya Amerika Jumatatu, Meja Chirchir alisema ni kweli majeshi ya Kenya yaliyoingia Somalia yanalengo la kuwasaka na kuwafukuza wapiganaji wa Al-Shabab, lakini hawakuhusika na mashmabulio ya Jumapili katika mji wa Afgoye.

Anasema, "nisingelipenda kuzungumzia zaidi ya hayo, labda baada ya siku mbili au tatu tutaweza kujua nini kilichofanyika."

Anasema kufuatana na habari walizopata ni kwamba kambi moja ya mafunzo ya Al-Shabab ilishambuliwa na silaha walizopokea hivi karibuni kutoka Baidoa ziliharibiwa, pamoja na baadhi ya makamnda wa kundi hilo huwenda waliuwawawalipokua wanakutana karibu na kambi hiyo.

Mashahidi huko Somalia wanasema walishuhudia miripuko mikubwa karibu na mji wa Afgoye uliyoko karibu km 30 kutoka Mogadishu.

XS
SM
MD
LG