Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:32

Shambulizi la guruneti lajeruhi 14 Nairobi


Mlipuko wa guruneti nchini Kenya wajeruhi watu 14, Jumatatu
Mlipuko wa guruneti nchini Kenya wajeruhi watu 14, Jumatatu

Mlipuko wa guruneti katika klabu moja mjini Nairobi umewajeruhi watu kadhaa, mapema Jumatatu

Watu wasiopungua 14 wamejeruhiwa wakati guruneti liliporushwa ndani ya klabu moja ya usiku katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Mlipuko wa mapema Jumatatu umekuja wiki moja baada ya Kenya kufanya operesheni ya kuvuka mpaka dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab wenye uhusiano na al-Qaida huko kusini mwa Somalia, baada ya wimbi la utekaji nyara wageni kwenye ardhi ya Kenya. Ubalozi wa Marekani nchini Kenya ulionya Jumamosi kutokea shambulizi la kigaidi nchini Kenya.

Marekani haikuelezea nani huenda akafanya shambulizi kama hilo, lakini ilisema inaonekana zinalengwa sehemu ambazo zitawajumuisha wageni kama vile madukani na klabu za usiku.

XS
SM
MD
LG