Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:26

Kenya yaendelea kupambana na ukeketaji


Msichana wa kimasai ameshika bango akipinga ukeketaji wanawake (FGM) nchini Kenya.
Msichana wa kimasai ameshika bango akipinga ukeketaji wanawake (FGM) nchini Kenya.

Februari 6 ni siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji wanawake na wasichana kote duniani. Siku hii ambayo hujulikana kama ‘Internationa Day of Zero Tolerance for Female Genital Mutilation” ni tukio ambalo hufadhiliwa na Umoja wa Mataifa.

Ukeketaji wanawake barani Afrika ni utamaduni wa enzi na enzi ambao unahisisha kukata baadhi ya sehemu za siri za wasichana wadogo na wanawake.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takriban wasichana na wanawake milioni 200 wamepitia utaratibu wa FGM, ikiwemo milioni 44 wenye umri wa miaka 14 au wadogo zaidi.

Rahma Wako mwenye umri wa miaka 50 alipitia utamaduni huu akiwa na umri wa miaka sita.

“Nilikatwa na baadaye kushondwa nikiwa na umri wa miaka sita. Walitumia chuma cha moto na kukibandika pale waliponikata, na ilichukua siku 40 kupona,” anasema Rahma na kuongezea kuwa katika siku hizo 40 alipata shida sana kwenda haja ndogo na kubwa, na hata kama ataishi mpaka umri wa miaka 100 bado anaikumbuka siku hiyo kama vile ndiyo kwanza amefanyiwa ukeketaji.

Miaka sita baada ya tukio hilo, wazazi wake walimuozeshwa kwa mwanamme mwenye umri wa miaka 70.

Alikumbwa na madhila na matatizo mengi katika ndoa yake. Alijaaliwa kujifungua watoto mapacha lakini alikumbana na matatizo mengi ya kiafya.

Rahma anasema wakati wa kujifungua alichanika kama vile nguo inavyochanika kwasababu alipofanyiwa ukeketaji walimshona sehemu yake ya siri kama nguo. Mara baada ya kujifungua alilazimika kushonwa stichi 28 na ilikuwa kazi kuuguza kidonda hicho.

Baada ya miezi sita, Rahma alishika mimba tena na kujifungua tena watoto mapacha. Kutokana na hilo aliamua kuondoka kwa mume wake, hivyo Rahma akadai talaka, alishinda kesi ya kupewa yeye watoto wake wanne awalee mwenyewe. Ameapa kuwa kamwe hataolewa tena na amekuwa ni mwana kampeni mkubwa kupinga ukeketaji.

Rahma anasema, “nilionekana msaliti katika jamii, nikipambana dhidi ya utamaduni wetu na hiyo ilinipa nguvu ya kupigania haki za wasichana, niliweza kuwazuia wasichana wengi kupitia utamaduni wa ukeketaji na kuwaepusha na mateso ambayo mimi nimepitia.”

Amefanikiwa kuwaokoa mamia ya wasichana kupitia utaratibu wa kukeketa. Anasafiri kwenda maeneo mbali mbali nchini humo ambayo yajishughulisha na utamaduni huu. Anasema watu wengi wameanza pole pole kujiweka kando na utaratibu huu.

Mwaka 2016 ripoti ya UNICEF imebaini kuwa wasichana na wanwake katika nchi 30 wamepitia ukeketaji, zaidi ya nusu ni nchini Indonesia, Misri na Ethiopia.

Nchini Kenya asilimia tatu ya wasichana walio na umri wa chini ya miaka 15 wamepitia FGM. Utaribu ambao umepigwa marufuku nchini humo tangu mwaka 2001. Wale wanaogundulika kufanya utaratibu wa FGM wanaweza kupewa adhabu ya kifungo cha mpaka miaka mitatu.

Utaratibu kwa kawaida hufanywa na watu ambao hawajapatiwa mafunzo utalaamu wa afya, na hivyo wanaweza kusababisha wale wanaofanyiwa utaratibu huo kupoteza damu nyingi au kupata maambukizo. Katika siku za baadaye FGM inaweza kusababisha maumivu makubwa wakati wa kujamiana na pia kuleta athari wakati wa kujifungua.

XS
SM
MD
LG