Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 14:16

Watu 35 kutoka Ethiopia wakamatwa Kenya

Polisi wa Kenya wakishika doria kwenye moja wapo ya mitaa ya Nairobi.
Polisi wa Kenya wakishika doria kwenye moja wapo ya mitaa ya Nairobi.

Polisi wa Kenya, wamekamata watu thelathini na watano wanaoaminika kuwa raia wa Ethiopia, katika operesheni ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu.

Polisi wa Kenya, wamekamata watu thelathini na watano wanaoaminika kuwa raia wa Ethiopia, katika operesheni ya kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu.

Gazeti la Daily Nation limeripoti Jumatano kuwa operesheni hiyo ilifanyika usiku wa Jumanne mwendo wa saa tatu katika nyumba moja kwenye mtaa wa Ruai, viungani mwa mji wa Nairobi.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Nairobi, Japheth Koome, alisema kuwa watu hao walipatikana wakiwa ndani ya nyumba moja, bila vibali vya kuwa nchini Kenya.

Koome alisema kuwa wote hao watafunguliwa mashtaka kwa kuwa nchini kinyume cha sheria, akiongeza kuwa mwenye nyumba walimokuwa anaendelea kusakwa na polisi.

Koome alisema kuwa polisi wanashuku kwamba watuhumiwa hao walikuwa njiani kuelekea Afrika Kusini.

XS
SM
MD
LG